-->

Asikuambie mtu, ndoa tamu jamani-Meya

MWIGIZAJI na mchekeshaji wa Filamu Bongo, Meya Shaabani amesema kabla ya kuingia katika ndoa aliichukulia poa, lakini kwa sasa anaona utamu wake na kumfanya afurahie maisha.

Meya alisema maisha anayoishi kwa sasa ni ya furaha na amani tofauti na enzi za uselana hiyo imetokana na kuoa mke anayefanana naye na kupendana kila siku upendo ukitawala katika nyumba na kuwa sehemu ya baraka za kazi zake.

“Kwangu maisha ya ndoa ni matamu sana kwani mtu niliyeoana naye tunafanana kwa vitu vingi na kujikuta tukiishi maisha ya burudani na amani, huku tukifurahia zawadi mtoto wetu Tariq na kuwa wazazi bora,” alisema Meya.

Meya aliyeoana na Amina Shaaban alisema kwa namna maisha ya ndoa yalivyo matamu hafikirii kabisa kuchepuka kwa sababu kwanza sio dili, pia mkewe ni tulizo lake na kila kitu kwake kwa sasa kipo tambarare tangu awe kwenye ndoa.

msanii mya shabani akiwa na mkewake amina shabani katika sherehe yao muhimu ya kufunga pingu za maisha

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364