AT Awapa ‘Makavu Live’ Mapromota wa Muziki Bongo
Game ya Bongo imekuwa ikishikiliwa na wasanii wa kutoka Tanzania bara na kwa sasa wasanii wengi wa kutoka Zanzibar wamekuwa wakifeli.
Akizungumzia sababu kubwa ya kufeli kwa wasanii hao Star wa mduara AT alisema kuwa mapromota ndo wanaoua vipaji vya wasanii hao.
“Wao wanapromote sana wahuni kuliko wastaarabu wanaojua kufanya kazi na ndomana muda mwingine tunaamua tukae pembeni kwanza muwapromote wahuni mukichoka mtakuja kwa wastaarabu tutaendelea na kazi zetu”, alisema AT
eatv.tv