Kutokana na kusuasua kwa hatua za tasnia ya filamu Bongo kuingia katika soko la kimataifa, nyota wa filamu Aunt Ezekiel amesema kuwa zipo jitihada zinafanyika sasa kuweka mambo sawa katika soko la ndani ambalo limeshuka, kama msingi wa safari hiyo.
Aunt ambaye hakufafanua mikakati yenyewe, ameeleza kuwa itakuwa ni uongo pale kufanya jitihada za kwenda nje ya nchi kukiwa na tatizo hapa nyumbani, akiamini kuwa bado tansia nzima haijachelewa kuchukua hatua hiyo muhimu licha ya kukua sana kwa utandawazi na pia teknolojia inayotoa njia za sanaa, wadau na wasanii kufanya hivyo.
Kwa sasa msanii huyo ana kazi mpya inayokwenda kwa jina “Saa Mbovu” inayobeba kisa chenye mafunzo kuhusiana na malezi ya watoto, binafsi sasa akiwa ni mama wa binti mmoja mwenye miezi 8 – Cookie.
Comments
comments