-->

Aunty Ezekiel Katuachia Funzo Juu ya Mapenzi

Moja kati ya matatizo ya watanzania, ni kushindwa kusimamia yale tunayoayaamini. Linapokuja suala la mapenzi wengi hujikuta kwenye wakati mgumu hasa ikiwa yule anayempenda anaonekana si wa maana mbele za watu kwa hadhi,kipato na muonekano.

Pengine mwaka 2016 mwanadada Aunty Ezekiel alituachia funzo,ukipenda usiangalie wengine wanaonaje fuata moyo wako na wasipooelewa wengine wataelewa mwisho wa safari.

Miaka michache nyuma ilisemekana mmoja kati ya warembo A-list wa bongo movie Aunty Ezekiel amebeba mimba ya dansa wa kutegemewa wa Diamond Platinumz, Mose Iyobo, haikuaminika na wengi wetu. Sio kwa kuwa Iyobo hatakiwi kupendwa, lahasha ila kwa kuWa imezoeleka mastaa hasa wa bongo movie kudate na watu wenye kipato kikubwa pengine na umaarufu mkubwa. Wengi waliamini Iyobo ni kama amewekwa kupoteza maboya ili watu wasimjue muhusika haswa wa mimba ya Aunty!

Miaka imepita Mose na Aunty wana mtoto wa kike anaitwa Cookie! Unajua nini? Ukipitia kwenye mitandao ya kijamii moja kati ya couple ambaye sasa zinazopostiwa sana ni Mose na Aunty,watu wanawatamani,watu wanaona wanapendezana.

Ingekua Aunty amewasikiliza pengine kusingekuwa na uhusiano. Ingekuwa amemuona kwa jicho wanalomuona wengine pengine penzi lingekufa siku nyingi. Lakini kwa kuwa alimua kuufuata moyo wake na kuamini kuwa yule ambaye wengine wanamuona sio sahihi kwake ndiye haswaa anastahili kukabidhiwa mtima wake,ndio sababu wapo walipo.

Kwa yoyote anayehusika, mapenzi ni baina ya nafsi mbili zinazopendana,ni vema kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi lakini maaumizi yabaki ya kwako. Mwisho wa siku wewe ndo unajua sababu ya kumpenda uliyenaye. Haijalishi wanasemaje au wanaonaje juu ya uhusiano wako Shika uliposhikilia kama kuelewa,wataelewa mbele wa safari.

Imeandikwa na Eliezer Gibson aka Green City Native

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364