Artists News in Tanzania

Avamia Mghahawa Zanzibar na Kuchoma Watu visu

Zanzibar. Watu sita wakiwemo wanne raia wageni kutoka nje ya Tanzania wamejeruhiwa vibaya kwa kuchomwa na kisu usiku wa kuamkia leo katika mgahawa wa Lukman Mkunazi Mjini Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali alizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake leo amesema kuwa tukio hilo limetokea saa 1:20 usiku wa kuamkia leo.

Kamanda huyo amesema kuwa mtuhumiwa aliyetenda tukio hilo ambaye jina lake halijatambulika ila kwa sura anafahamika, anakisiwa kuwa na umri wa miaka (25) ambapo hadi wakati huu bado hajapatikana.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wao wa awali wamebaini kuwa mtuhumiwa huyo amefika katika mgahawa huo na kuwachoma watu watatu ambao walifika mgahawani hapo kwa ajili ya kujipatia chakula.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Mauget Gerarol (66) raia wa Ufaransa ambae amejeruhiwa pembeni ya jicho lake la kulia, Jennifer Wolf (24) raia wa Ujerumani aliejeruhiwa katika sehemu yake ya kichwa na Anna Catharina(20) raia wa Ujerumani aliejeruhiwa kichwani.

Kamanda huyo alisema baada ya mtuhumiwa huyo kuwachoma visu watu hao alikimbia na akiwa njiani umbali wa mita 60 kutoka eneo la tukio la awali njiani alikutana na kijana wengine waitwao Hassan Abdallah mkazi wa Kiponda (24) na raia wa Canada, Liying Liang na kuwajeruhi kwa kuwachoma kisu mdomoni na shavuni.

Alisema pamoja na kuwachoma watu hao lakini walifanikiwa kuwachoma visu Sajad Hussein (55) ambapo majeruhi hao wote walikimbizwa hospitalli ya Tasakhtaa Global iliyopo Majestic kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Alisema kuwa majeruhi hao wote walipatiwa matibabu na kuruhusiwa lakini Mauget Gerarol raia wa ufaransa bado amelazwa hospitalini hapo na anaendelea kupatiwa matibabu.

 Mwananchi

Comments

comments

Exit mobile version