Wanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii Kocha) wametoka jioni hii katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kulakiwa na familia na mashabiki wao.
Taarifa zaidi baadaye.
Mapema leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, alitangaza msamaha kwa wafungwa wakiwemo Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) ambao walifungwa jela maisha mwaka 203 katika Gereza la Ukonga ambap rais aliagiza waachiwe huru mara moja kutoka gerezani.
Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.
Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.
Chanzo:GPL
Comments
comments