Babu Yake Wastara Aeleza kilichosababisha Ndoa ya Wastara Kuvunjika
Babu yake Wastara amefunguka na kueleza kilichosababisha kuvunjia kwa ndoa ya Wastara na Mbunge wa Donge kupitia CCM Sadifa Khamis Juma.
Akizungumza na Times Fm, Babu huyo aliweka bayana kuwa Mbunge huyo mwenye cheo ndani ya umoja wa vijana CCM, alifikia hatua ya kuwatongoza wafanyakazi wa ndani ili awe nao kimapenzi.
“Wastara hataki kurudiana na Sadifa, kutokana na vitendo alivyokuwa akivifanya, imefikia wakati mpaka wale wafanyakazi wa ndani wananambia babu, babu, baba huku anatutongoza njoo uone na meseji tunazo kwenye simu,” alisema Babu.
Aliongeza, “Alafu hana adabu anafikia hatua ya kuniambia mimi nalala na mtoto wangu Wastara, aisee sijui atakuja kunieleza vipi kwa hilo”
Aidha ameweka bayana kuwa, kwa sheria za Dini ya Kiislamu ndoa hiyo siyo halali mara baada ya Mbunge huyo kutamka hadharani kwamba amemuacha Wastara.
Bongo 5