Msanii Baraka The Prince ambaye kwa sasa yupo chini ya lebo kubwa ya muziki Afrika ya Rock Star, ametangaza ujio wa recording lebel yake, itakayosimamia kazi za wasanii wengine.
Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT ya East Africa Television, Baraka aliulizwa kuhusu maana ya jina la BANA ambalo analitumia, ndipo akafunguka na kusema kuwa jina hilo ni kifupi cha jina lake na la mpenzi wake Najma, na pia ndilo jina la kampuni yao itakayosimamia vitu mbalimbali ikiwemo recording lebel.
“BANA ni Baraka and Najma, ni kampuni itakayokuwa na vitu vingi vingi, kutakuwa na recording lebe, itakuwa na masuala ya mavazi, yani tunataka kutengeneza nguo ambazo zina lebel yetu, na pia kutakuwa na masuala ya chakula humo humo, so ina mambo mengi mengi tofauti”, alisema Baraka the Prince.
Baraka alisema recording lebel hiyo haitasimamiwa na yeye mwenyewe kutokana na majukumu mengi aliyonayo ya kimuziki, isipokuwa kutakuwa na watu ambao watasimamia kazi hizo zote pamoja na wanasheria.
“Ujue kusimamia wasanii siyo mimi ndo nitakuwa nipo front sana, kutakuwa na mameneja, kila msanii atakuwa na meneja wake, ina maana mimi sitakuwa nahusika moja kwa moja na wasanii, ila nitakuwa kwenye management”, alisema Baraka.
Iwapo Baraka atafanikiwa kuanzisha lebo hiyo atakuwa anaungana na wasanii wenzake kama Diamond, Nahreel na Barnaba, kwa kuanzisha recording lebel zao wenyewe.
eatv.tv
Comments
comments