Muigizaji wa filamu nchini, Yobnesh Yusuph, Batuli’ amesimama na kutaka watu waiheshimu sanaa ya Tanzania na kuwatetea wasanii kwamba hawahusiki na suala la upigaji picha za utupu isipokuwa watu wachache waliojipenyeza kwa staili ya picha.
Batuli ametoa kauli hiyo kipindi hiki ambacho wasanii wa magizo na muziki wamekuwa wakinyooshewa vidole na serikali kwa kuvaa mavazi yasiyo na maadili na kuweka picha kupitia mitandao na hata kwenye kazi zao za sanaa.
Batuli amesema kwamba idadi kubwa ya watu hao wanaotupia picha za uchi mitandaoni hawapo kwenye sanaa ya uigizaji isipokuwa jaamii isiyo na maadili kuwapokea kwa shangwe.
“Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu kwenye mitandao hawapo kwenye makundi haya mawili… muziki na filamu, umaarufu wao wameupata kwa kupiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii na watanzania wasio na maadili kuwapokea kwa shangwe,” Batuli
Siku chache zilizopita Naibu Wazirio wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni alitangaza kuwashughulikia wasanii wasiofuata maadili ya nchi ikiwa ni agizo la Rais Magufuli la wasanii kufuata maadili ikiwa ni pamoja na mavazi.
EATV.TV
Comments
comments