Artists News in Tanzania

Belle 9: Siwezi Kufanya Singeli, Atoa Sababu

Belle 9 amesema hafikirii kabisa kufanya muziki wa Singeli. Muimbaji huyo wa R&B amesema huo ni muziki wa kupita na katu hauwezi kudumu.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM, Prince Ramalove iwapo atafanya muziki huo mashabiki wakimtaka.

“Sitegemei,” alisema Belle.

“Hata kama nitafanya, sitofanya kama release song sababu Singeli ni muziki fulani hivi ambao unapita, ni bubble gum music. Sasa hivi watu wanaushabikia lakini itafika time utapita, sio muziki wa kustick.”

Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version