Ben Paul: Wanaume Msikatae Mimba
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’, amewataka wanaume wakware kutokutaa mimba kwa sababu kufanya hivyo wanasababisha vifo vya watoto wasio na hatia.
Ben Pol alisema wasichana wengi wanatoa mimba kutokana na kukataliwa na wanaume wanaowapa mimba hizo.
“Kuitwa baba ni raha sana jamani watoto ni sehemu kubwa ya faraja, mimi kila siku najiona mpya, lakini kitendo cha wanaume wenzangu kuwapa mimba wanawake na kuwakataa ni kitendo cha aibu na cha kishamba,” alisema Ben Paul.
Aliongeza kuwa angependa kuwaona wanaume wenzake wakijali familia zao ili wasisababishe vifo vya watoto wasiokuwa na hatia.
Mtanzania