-->

Bi Hindu Atoboa Sababu ya Bongo Movie Kuporomoka, Uhawara Kazini Huchangia

Muigizaji mkongwe wa filamu za kibongo Bi Hindu amefunguka na kusema kuwa tasnia hiyo ya filamu nchini inazidi kuporomoka na kushuka kwa kasi sababu watu wamesahau misingi ya kazi hiyo na sasa wanafanya utani huku wengine wakiendekeza mapenzi na kuacha vipaji.

Bi Hindu3

Bi Hindu alifunguka hayo kwenye kipindi cha eNEWS na kusema kuwa baadhi ya waongozaji wa filamu hizo wanaendekeza mapenzi na kuwapanga mahawara zao kwenye filamu ambao hawana vipaji na hicho ndiyo chanzo kuoneka tasnia hiyo imepoteza mwelekeo.

“Siku hizi watu hawaangali vipaji tena, unakuta baadhi yao wanawapanga mahawara zao na kuwapanga kwenye kazi zao, hivyo unakuta wale wasichana hata kucheza picha wanaringa, hata ukisema wanaleta dharau sababu unakuta wanatoka kimapenzi na wakubwa ya hizo kazi, mimi naitaka kazi hii ichukue maadili kama zamani sababu huko mbele tunakoelekea watu wanaweza kucheza uchi” alisema Bi Hindu

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364