-->

Bi Mwenda: Agoma Kufungukia Uchawi, Mme Na Watoto

Katika kolamu hii tunayowaletea wasanii mbalimbali wa filamu kila wiki, leo tunaye nguli wa filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Chau’ ambaye pia aliwahi kutamba katika Kundi la Kaole lililokuwa na ‘vichwa vikali’ kama vile marehemu Steven Kanumba, Ray, Muhogo Mchungu, Kipemba, Dk. Cheni, Mtunisi, Frank, Nina, Nana, Norah, Kibakuli, Nyamayao, Max, Zembwela, Bambo, Kingwendu, Swebe, Zawadi na wengine wengi.

BI MWENDA

Bi Mwenda amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake kama alivyoulizwa na wasomaji wetu.Msomaji: Una muda gani tangu uanze sanaa na imekunufaisha vipi?
Bi Mwenda: Nimeanza sanaa ya uigizaji mwaka 1998 na kusema kweli imeninufaisha sana, nimesomesha na pia nimejenga Musoma.

Msomaji: Mara nyingi huwa nakuona kwenye usafiri wa daladala tofauti na wasanii wakubwa wengine ambao hupendelea kuwa na usafiri wao na wengine kukodi usafiri binafsi, uhofii hadhi yako kushuka?

Bi Mwenda: Nihofie nini kwa mfano! Napenda kupanda daladala sababu hao wanaopanda ni binadamu kama mimi japokuwa nikijisikia huwa napanda Bajaj na bodaboda.

Msomaji: Vipi unaishi na mumeo na una watoto wangapi hadi sasa?
Bi Mwenda: Jamani umri huu wa kuniuliza nina mume na mambo ya watoto? Unataka unioe wewe?

Msomaji: Nilikuwa napenda filamu zako za kichawi, mbona siku hizi huchezi hivyo?
Bi Mwenda: Kama wewe mchawi kacheze wewe! Mi nimeacha maana mashabiki wangu wanahisi labda ni mchawi kweli.

Msomaji: Kwa nini wasanii wengi wa filamu wanapenda maisha ya kujikweza kwa kujiona matajiri wakati siyo?

Bi Mwenda: Nahisi filamu kwa kiasi kikubwa zinachangia hilo maana mtu anaweza kuwa na maisha ya kawaida lakini akacheza tajiri na mwisho wa siku maisha hayo ya kitajiri akahamishia kiuhalisia.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364