Bongo Movie Haijafa- Batuli
KUNA wakati ambapo kila mtu huwa na lake la kusema katika kuongelea jambo linalogusa maslahi yake kama mwanadada msanii mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ anayepingana na kauli ambazo hutolewa na baadhi ya wasanii kuwa tasnia ya filamu imeshuka au inaelekea kaburini.
“Huwezi kubishana na mtu kuhusu kusema kuwa Bongo Movie imeshuka au imekufa ni mtazamo wa mtu lakini kwangu naona ipo hai na watu tunaendelea kufanya kazi kama kawaida na watu wanapata riziki kwa kifupi Bongo Movie haijafa,”alisema Batuli.
Batuli anasema kuwa ni vema watu kufanya utafiti na kuborersha sehemu zenye matatizo na kuwakatisha tamaa kwani bado wanwa wapenzi wengi wa kazi zao na wanawakubali kutia filamu na si kitu kingine, ukiona msanii anafanya biashara nyingine ni katika kujiongezea kipato kutokana na mfumo uliopo.
Filamu Central