Breaking : Raila Odinga ajitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio Kenya
Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, leo October 10, 2017 ametangaza kutoshiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao uliamriwa na mahakama kurudiwa October 26 mwaka huu.
Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.