-->

Burundian In Dar Kutikisa Afrika Mashariki

USHIRIKIANO wa wasanii wa Tanzania na Burundi inatabiriwa kufanya vinzuri sokoni kufuatia umahiri wa wasanii waliocheza katika filamu ya Burundian in Dar, akiongea na FC mtayarishaji wa sinema hiyo Sururu Jafar ‘Burundiano’ amesema kuwa kazi hiyo imekutanisha wasanii nyota Burundi na Tanzania.

Hemed akiwa na Jack Wolper wakiwa katika moja ya scene.

Stelingi Sururu Jafar katika pozi.

Burundiano katika pozi la picha .

Mr. Burundiano akiwa na Jack Wolper.

“Tunatarajia kutikisa Afrika Mashariki na filamu yetu kwani ni kazi ambayo inatukutanisha wasanii wakubwa kutoka Afrika Mashariki nipo mimi mwenyewe kuna Hemed, Jack Wolper na wasanii wengine,”alisema Mr. Burundiano.

Wasanii wakali kama Nancy Amie Fidelle, Nzeyimana Nasoro wapo katika sinema hii ambayo pia imerekodiwa katika nchi mbili yaani Burundi na Tanzania na kuongozwa na muongozaji mahiri wa filamu Afrika Mashariki Wise na imekamilika muda si mrefu itaingia sokoni.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364