Chemical: Sifagilii Masharobaro, Nataka Mgumu Kama Nay wa Mitego
Miongoni mwa marapa wa kike wanaofanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chemical ni miongoni mwao ambapo hivi karibuni ameonekana kwenye muonekano mpya wa ‘kisistaduu’ tofauti na alivyozoeleka.
Kufuatia wengi kumhoji kuhusu mwonekano huo mpya, mwanadada huyo amefunguka kwamba yeye siyo sistaduu n ahata kwenye suala zima la mapenzi, hawafagilii masharobaro bali anataka mwanaume mgumu kama Nay wa Mitego watakayeendana.
Chemical ametaja sifa za mwanaume anayemhitaji katika maisha yake pindi atakapokuwa tayari kuingia kwenye mahusiano na kuongeza kuwa akishampata na wakikubaliana, haraka sana akajitambulishe nyumbani kwao.
“Mimi ni msichana f’lani ambaye napenda mwanaume f’lani hivi mgumu lakini sijui nitakuja kuangukia wapi maana mapenzi hayachagui, lakini napenda sana nikutane na mgumu na siyo sharobaro, awe real kama Nay wa mitego vile,” amesema Chemical.
Chanzo:GPL