Chief Kiumbe Akinipa Ndinga Sikatai-Young Killer
Msanii Young Killer ambaye siku za karibuni ameachia wimbo wake mpya akiwa na Mr Blue amefunguka na kusema kuwa ikitokea Chief Kiumbe amempa gari hawezi kukata sababu hakuna mtu ambaye anapenda maisha ya shida au ya chini
Young Killer alisema haya kupitia kipindi cha eNEWS na kusema kuwa yeye kuwataja madoni kwenye wimbo wake haina maana kuwa amewashawishi ili wampe kitu, bali amefanya hivyo kwa mapenzi yake mwenyewe na kudai hata kama ikitokea kweli akapewa ndiga haiwezi kukataa.
Mbali na hilo Young Killer amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuwataja majina watu hao ni kwasababu wamemsaidia kimawazo, kwa kipindi ambacho alikuwa kimya hivyo amefanya hivyo kama kuwakumbuka na kuweka kumbukumbuka kwa kile walichomsaidia.
eatv.tv