Chuchu Hans: Naanza Kumwandaa Jaden Kuwa Staa
STAA wa Filamu za Bongo, Chuchu Hans, amesema kuwa atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha anamwandaa mtoto wake wa kiume kuwa staa wa baadaye.
Msanii huyo pamoja na Vicent Kigosi ‘Ray’ walifanikiwa kupata mtoto wa kiume mapema mwaka huu, ambaye amepewa jina la Jaden.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Chuchu alisema Jaden si wa kwanza, hivyo ili aweze kutimiza malengo yake ataingia mikataba na kampuni mbalimbali zitakazohitaji ubalozi wa mtoto huyo.
“Ifahamike mwanangu ni mtoto wa mastaa wawili hapa Bongo, hivyo namuomba Mungu aniweke ili niweze kumlea kifalme awe staa mkubwa na mwenye kuheshimika ndani na nje ya nchi,” alisema Chuchu.
Mtanzania