KUFUATIA madai kwamba dereva aliyeacha usukani na kukucheza wimbo wa ‘Muziki’ ulioimbwa na msanii Sharif Ramadhani ‘Darasa’ akishirikiana na Bernard Paul ‘Ben Pol’ huku gari likiwa katika mwendo kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhatarisha maisha ya wasafiri na watumiaji wengine wa barabara, msanii wa wimbo huo ametahadharisha mashabiki wake.
“Kilichotokea kwa dereva aliyeacha usukani na kucheza ilikuwa ni mzuka, mtu yeyote inaweza kumtokea, ila ni hatari kwa usalama wa maisha ya mali na watu wake, hivyo nawatahadharisha mashabiki wangu wawe makini wanapokuwa katika hali ya kupandwa mzuka wakiwa katika mazingira magumu ya kucheza, wajenge uvumilivu ili wasihatarishe amani,’’ alieleza Darasa, akiwa na furaha kutokana na wimbo wake huo kufanya vizuri.
Darasa aliwataka mashabiki wake wajifunze kupitia dereva huyo, akidai alichokifanya ni kizuri kwake kama shabiki, lakini ni hatari kwa wengine, hivyo angeweza kuzuia hisia zake isingetokea.
“Nafahamu kama kitu ni kizuri kinaweza kuwapa watu mzuka, lakini wanatakiwa kuangalia na mazingira waliyokuwepo, kwani inaweza ikasababisha madhara makubwa, mfano huyo dereva angeweza kupata ajali ikasababusha madhara makubwa,” alisema.
Licha ya kutamba na wimbo huo, Darasa anatamba na wimbo wa ‘Too Much’.
Mtanzania
Comments
comments