Artists News in Tanzania

Davina Alia Filamu za Mapenzi Kuua Soko

Muigiza wa long time Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameibuka na kueleza kwamba filamu za mapenzi wanazocheza wasanii wengi zimeua soko ndiyo maana kwa sasa ni kama sanaa hiyo haipo.

Akichonga na paparazi wetu hivi karibuni, Davina alisema kutokana na soko la filamu kuwa gumu wasanii wengi wameamua kugeukia biashara kwani wakikaa na kusubiria sanaa hiyo watakufa njaa.

“Tunapigana ili tulirudishe soko la filamu liwe kama zamani maana limekufa kutokana na filamu za mapenzi tunazocheza mara kwa mara. Kuna kila sababu ya kubadilika kama kweli tunataka kulishika soko,” alisema Davina.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version