STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amedai kuwa anatamani Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uendelee kwani umepunguza misengenyo baina yao tofauti na wakati mwingine katika mwaka.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Davina alisema anatamani Mwezi Mtukufu ungeendelea kwa sababu umekuwa wa amani na utulivu, pia watu wamekuwa wakitenda mema, kujisitiri kwa mavazi ya heshima hasa wasanii.
“Natamani sana Mwezi Mtukufu ungeendelea lakini ndiyo hivi unaishia, niwatake wasanii wenzangu na watu wote waendelee kutenda mema, siyo wakarudie maisha ya zamani ya kufanya mambo yasiyompendeza Mungu,” alisema Davina
Chanzo:GPL
Comments
comments