NYOTA wa filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’ amemtaka Waziri Mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, Nape Moses Nnauye ili kuwasaidia wasanii.
“Tunamuombea Mungu Waziri Mwakyembe awe nasi karibu kama alivyokuwa Nape, kwani tulikuwa tukimpigia simu na kumweleza shida zetu za sanaa, muda wote anapokea mwenyewe, tunamuomba waziri wa sasa asituwekee ugumu wa kumuona au kuzungumza naye, ili aweze kutusaidia changamoto mbalimbali zinazotukabili pia aendeleze yale aliyoanzisha waziri aliyekuwepo,” alisema Davina.
Davina alisema ni vyema kama Mwakyembe akawa bega kwa bega na wasanii kwani hali ya sasa ni mbaya katika sanaa yao hivyo wanahitaji mtu wa kuwa karibu nao kama alivyokuwa Nape.
Chanzo: GPL
Comments
comments