Diamond Afunguka Haya Baada ya Profesa Jay Kumsemea Bungeni
Msanii Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz leo kupitia akaunti yake ya Instagram ameeandika maneno yanayoashiria kutokufurahia hotuba ya mbunge wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Prof Jay.
Diamond aliandika maeno hayo yanyosomeka “Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo….. @professorjaytz
Pro .Jay katika hutuba yake leo bungeni alizungumzia pia suala la msanii huyo kudaiwa kodi na TRA milioni 400, akiitaka serikali iangalie upya kwani wanashindwa kutambua mchango wa wasanii baada ya kampeni zao.