Artists News in Tanzania

Diamond afunguka kuhusu mahusiano na baba yake mzazi (+video)

Baada ya tetesi za muda mrefu kuzagaa kuwa Msanii wa Muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz kuwa hana mahusiano mazuri na baba yake mzazi, Hatimaye Diamond ameweka wazi ukweli wote kwa kukanusha taarifa hizo.


Diamond amesema kuna watu wenye hira ndio wanaokuza mambo lakini yeye huwa anawasiliana naye na huwa anamsaidia pale anapokuwa na kitu.

Ingawaje Diamond amekiri wazi kwamba hana mazoea naye kama ilivyo kwa mama yake mzazi lakini hakuna bifu kama baadhi ya watu wanavyokuza mambo.

Kwa upande mwingine, Diamond amewakanya baadhi ya watu ambao wanampeleka baba yake hadi kwenye geti lake na kumpiga picha ili kuupotosha umma kuwa amemfungia geti baba yake, waache hiyo tabia kwa sababu inaathiri hadi familia nyingine. Tazama video ya Diamond akizungumza tukio hilo hapa chini


Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version