Kumekuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuhusiana na ‘video Queen’ wa ngoma mpya ya Raymond Tip Top iitwayo ‘Kwetu’ aitwaye Lyyn kuwa anatoka na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Kwa muda wa wiki kadhaa Diamond alikuwa kimya kuhusiana na taarifa hizo lakini siku ya jana kupitia akaunti ya Instagram aliwajibu wanaojaribu kumuachanisha na mpenzi wake Zari na kuandika haya mara baada ya kuweka picha ya Zari.
“Roho ya SIMBA!!!…. wanajaribu ila hawatokaa Waweze… Nakupenda Mpaka Naugua! @Zarithebosslady ? #Mmechelewa”
Comments
comments