Diamond Azima ‘Cheche’ ya Ommy Dimpoz
Diamond Platnumz amedondosha nyimbo mpya akiwa na wakali wa raga kutoka Marekani, kundi la Heritage Morgan.
Ngoma hiyo inayotambulika kwa jina la Halelujah imeonekana kupokelewa vyema na wadau wa muziki ambapo mpaka sasa katika mtandao wa Youtube imeweza kukusanya watazamaji zaidi ya laki tatu.
Kama kawaida wengine wameanza kusema kuachiwa kwa ngoma hii ni sababu Diamond anataka kuzima video ya Ommy Dimpoz ya wimbo wa Cheche ambayo mpaka jana ilikuwa namba moja katika video zilizotazamwa zaidi.