Artists News in Tanzania

Diamond Platnumz Afunguka Kuwauzia Mitumba Ali Kiba na Bob Junior

Msanii Diamond Platnumz anasema kabla hajatoka kimuziki alikuwa anafanya biashara ya kuuza mitumba na biashara hiyo ndiyo iliweza kumkutanisha na ‘Producer’ Bob Junior ambaye aliyetengeneza kazi zake za kwanza ambazo zilimtambulisha kwa watanzania.

Diamond Platnumz alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikuwa anapenda sana kumuonyesha onyesha nguo Bob Junior na wenzake ili aweze kupiga pesa kutoka kwao.

“Unajua mimi nilikuwa nakutana sana na BOb Junior pale kwao ilipokuwa ‘studio’ kwa sababu nilikuwa nauza nguo maeneo yao pale, sasa yeye alikuaga anapita na kina Ali pale nawaonyesha onyesha nguo najua hawa ma brazameni ili mimi nipige hela’ alisema Diamond Platnumz

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version