Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekiri kuzaa mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Amezungumza hayo leo Jumanne akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha televisheni na redio cha Clouds na kusema mtoto ‘Abdul’ ni wa kwake.
“Mimba ni yangu na sitokaa nikaachana na Zari,” amesema Platnumz.
Ambapo amesema amemgharamia Hamisa pamoja na mtoto tangu kipindi cha ujauzito wake mpaka mtoto anazaliwa ili kuhakikisha mama na mtoto huyo wanakuwa salama.
Amesema pamoja na yaliyotokea alimwambia mama yake mzazi kuhusu kilichotokea amemuomba msamaha Zari na hawana shida yoyote.
“Mimi ni mwanadamu na kilichotokea kimetokea na niko tayari kumhudumia mtoto,” amesema Diamond.
Diamond amesema kuwa alimuonya Hamisa kutokumtukana Zari kwani hausiki na chochote kilichotokea na badala yake ajishughulishe na mambo mengine.
Comments
comments