Diamond amesema wakati anaanza muziki, alikuwa anamuigiza Barnaba lakini baadaye akaja kupata njia yake mwenyewe.
Alisema hivyo kujibu swali la anaonaje pale anapomsikia Harmonize akiimba kama yeye.
Akiongea kwenye kipindi cha The Base cha ITV, Diamond alisema, “Unajua katika muziki kila mtu ana role model wake. Mimi wakati naanza nilikuwa nawaangalia sana Ne-Yo na Usher Raymond na kwa hapa nyumbani nilikuwa namkopi sana Barnaba maAna ndIo msanii ambaye nilikuwa nampenda. Lakini baadaye nikaja kuwa kama mimi. Kwahiyo Harmonize naye ndio hivyo atakuja kuwa kama yeye tu na sidhani kama anaimba kama mimi,” alisisitiza.
Kwa muda mrefu, Harmonize amekuwa akilalamikiwa kwa kumgeza sana bosi wake huyo.
Bongo5
Comments
comments