Diana Ajipanga Kumuombea Lulu
STAA wa filamu Bongo, Diana Kimari, amesema anajipanga kwenda Gereza la Segerea jijini Dar kumuombea aliyekuwa swahiba wake, Elizabeth Maichael ‘Lulu’ anayetumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Akizungumza na gazeti hili, Diana alisema kuwa, zaidi ya mara tatu alishajipanga kwenda gerezani kumuona lakini hakuweza kufanikiwa kutoka na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake Ingawa kwa sasa amejipanga kwenda na wadada ambao kila mwisho wa mwezi wanaenda kuwapa Neno la Mungu wafungwa.
“Sio kwamba nipo kimya simkumbuki Lulu, hapana! Mwisho wa mwezi huu najipanga kwenda kumuona kuna wadada ambao huwa wanaenda kutoa Neno kila mwisho wa mwezi gerezani ndio nitaenda nao na ninajua wazi atafurahi sana,” alisema Diana ambaye ni muumini katika kanisa la Mchungaji Mwamposa.
Chanz0:GPL