Dimpoz Mikononi Mwa Polisi Dar Masaa Matano
STAAA wa Bongo Fleva nchini, Ommy Nyembo aka ‘Dimpoz’, ambaye anatamba na kibao chake cha ‘Cheche, jana alikuwa kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam kunako saa tano asubuhi akiwa amesindikizwa na watu wengine wawili.
Alipohojiwa na mtandao huu baada ya kutoka kituoni hapo, Dimpoz alisema: “Niliitwa kwa ajili ya mahojiano lakini mambo mengine yapo chini ya polisi. Nitaweka mambo yote sawa lakini si sasa maana siruhusiwi kuongea chochote juu ya hili, ” Dimpoz alisema.
Mwanamuziki huyo aliingia kituoni hapo wakati waandishi habari wakienda hapo kwenye mkutano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Hata hivyo Kamanda Mambosasa kwenye taarifa yake ya mchana kwa waandishi wa habari hakuzungumzia chochote kuhusu Ommy Dimpoz kuhojiwa lakini taarifa za kiundani zaidi ambazo hazijathibitishwa, zinasema Ommy aliitwa kutokana na picha aliyoi-post kwenye mtandao akiwa na mama mzazi wa mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Platimumz.
NA SAMSON JEREMIAH/GPL