Msanii wa bongo fleva Dito amesema amekaa na mwanamke wake kwa miaka mitano na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume lakini bado hawajafanikiwa kufunga ndoa.
Akiongea ndani ya eNewz Dito amewapongeza wasanii waliofunga ndoa na kusema wamefanya vizuri kutengeneza familia ambazo baadaye zitawasaidiaa kwa kuendeleza vipaji kupitia watoto wao au kuwa wasimamizi wa muziki wanaoufanya na kusema mambo yake yakiwa sawa atafunga ndoa.
Hata hivyo Dito amewashukuru mashabiki zake kwa kuendelea kumsapoti katika muziki wake pamoja na kukaa muda mrefu bila kutoa nyimbo lakini alipotoa ngoma yake mpya ya moyo sukuma damu amepata sapot ya kutosha.
eatv.tv
Comments
comments