Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Lameck Ditto amesema muziki wake bado unamlipa zaidi kupitia ring tone na hiyo ndio ilikuwa shabaha yake; kufanya nyimbo ambazo zitaishi kwa muda mrefu.
Akiongea na Clouds E ya Clouds TV, Ditto alisema, “Unajua licha ya kuwa kimya kwa muda ila nyimbo zangu huwa zinakaa muda mrefu. Mtu akisikiliza kama ‘Tushukuru kwa Yote’, au ‘Wapo’ akienda katika maharusi utasikia na katika mioyo ya watu bado zipo.”
“Kwahiyo huwa naziacha ziendelee kuishi. Unajua watu wanaamini masoko katika sehemu nyingine lakini masoko yapo sehemu nyingi pamoja na kuwa kuna challange tofauti tofauti. Ila namshukuru Mungu katika miito ya simu (RBT) huwa kuna kipato kinaingia kutokana na kazi zangu kidogo japo huwa kinapanda au kinashuka,” aliongeza.
“Lakini hiyo ndio ilikuwa hasa target yangu, nina imani hizo challenge ambazo zipo zingeshughulikiwa kipato kingekuwa kikubwa zaidi. Sasa karibu miaka minne au mitano hivi naona zinafanya vizuri nyimbo zangu katika ring tone, naona huko hasa ndio soko la nyimbo zangu lilipo.”
Bongo5
Comments
comments