Dkt. Shika Afunguka Kuyatosa Matangazo, Atoa Sababu
Dkt. Lous Shika amesema hivi sasa hataki kufanya matangazo ya biashara kama ilivyokuwa awali, akisema kwamba anahofia usalama wake.
Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo ataendelea kufanya dili za matangazo itakuwa rahisi kwa watu wanaomtafuta kujua yuko wapi.
“Sina interest na haya matangazo tena kwa sababu wale warusi niliowakimbia watanitrack watajua niko wapi, lakini natoa ushirikiano kwa wenzangu huku nikiwa nimetafuta means nyingine za kuwakwepa”, amesema Dkt. Shika.
Dkt. Shika amesema watu hao ambao walimteka na kumtesa nchini Urusi, kawaida yao huwa hamuachi mtu salama bila kuhakikisha wamempoteza kabisa, wakihofia nao kujulikana.