-->

Dogo Mfaume Amefariki Akiwa Anasubiri Upasuaji

Dar es Salaam. Kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Mfaume Selemani maarufu kama Dogo Mfaume, kimekuja ikiwa ni siku chache tangu Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla kutoa msaada kwa ajili ya matibabu ya uvimbe karibu na ubongo uliokuwa unamsumbua.

Mfaume Selemani maarufu kama Dogo Mfaume,

Dogo Mfaume aliyewahi kutamba na wimbo ‘Kazi yangu ya dukani ‘, amefariki leo (Jumanne) katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) alipokuwa amelazwa akiendelea na matibabu.

Mmiliki wa kituo cha Pili Misana Back To Life sober house kinachotoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya, Pili Misana amesema Kigwangalla alitoa msaada huo baada ya fedha za matibabu kukosekana.

“Dogo Mfaume alikuwa akisumbuliwa na maradhi tangu mwanzoni mwa mwaka huu na baadaye iligundulika kuwa na uvimbe karibu na ubongo na hapo ndipo Naibu Waziri akatupatia msaada tukaanza matibabu Muhimbili,” amesema.

Amesema wiki hii Dogo Mfaume alikuwa amelazwa Muhimbili akisubiri kufanyiwa upasuaji Ijumaa.

“Kesho tulitakiwa twende hospitali kwa ajili ya kumtolea damu, lakini kwa bahati mbaya amefariki,”amesema.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364