Dokii Afunguka Kukosa Madili, Atoa Wito Huu
Muigizaji wa filamu na mwanamuziki nchini maarufu kwa jina la Dokii, amefunguka na kusema kuwa tangu alipo tangaza kuokoka amekuwa akikosa madili mengi sana kwenye tasnia ya filamu nchini.
eNewz ilipiga story na Dokii na alisema amekuwa akikosa kazi za u ‘MC’ na sanaa aliyokuwa akiifanya kutokana na watu wengi waliokuwa wakivutiwa na ukataji wake wa viuno kitu ambacho wengi wanafikiri kwasasa hawezi kufanya tena.
“Watu wamepungua sana kunipa kazi kwa sababu nimeokoka, nimekuwa nikikosa kazi nyingi za uigizaji katika scene tofauti tofauti za mapenzi kisa nimeokoka pia hata kwenye kazi yangu ya u ‘MC’ ambapo muda mwingine nilikuwa nakata sana viuno ili kufurahisha watu lakini sasa hivi sizipati kwa sababu watu wanahisi mtu ukiokoka kuna vitu hufanyi, mimi naweza kwa sababu ile ni kazi yangu hata kama nimeokoka nitafanya tu kwa sasabu hata Mungu naona kuwa ni kazi na nafanya kwa sababu ya kuelimisha jamii”
Hata hivyo Dokii alimalizia kwa kusema kuwa, mbali na kuokoka yeye anafanya kazi yake kama kawaida na watu wasisite kumtafuta kwa kudhani kuwa hataweza kufanya kama ilivyokuwa awali.
Dokii alijulikana zaidi kwa kuongea lafudhi ya Kikenya hadi kupelekea watu kuhisi kuwa ni Mkenya,