Dude Atoboa Siri ya Maisha Yake
KULWA Kikumba ‘Dude’ ametoboa siri ya maisha yake kuwa, tangu ajitambue hajawahi kuugua hadi kulazwa pia kupelekwa nyuma ya nondo kwa kosa lolote lile.
Dude alizungumza na Full Shangwe na kusema anamshukuru Mungu kwa kumlinda kwa mambo hayo mawili katika maisha yake.
“Tangu nimejitambua sijawahi kuugua hadi nikalazwa wodini au kupelekwa nyuma ya nondo kwa uhalifu wa aina yoyote ile. “Huwa naugua naenda kutibiwa na kurudi nyumbani kiaina. Si jambo la kawaida ila ninamshukuru sana Mungu,” alisema Dude