Artists News in Tanzania

Dudubaya:Muziki Siyo Mkojo

Msanii Dudubaya amefunguka na kusema kuwa msanii anapaswa kutulia na kujipanga kwenye kutengeneza nyimbo zake ili aweze kufanya kazi nzuri na yenye kuvutia kwa mashabiki kwani muziki si kama mkojo kuwa unapojisikia umekubana ukojoe.

Dudubaya amesema hayo kupitia kipindi cha eNEWS alipokuwa akielezea sababu za yeye kuendelea kutamba na kuzungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo mbalimbali ili hali hana kazi mpya yoyote kwenye Radio au Television.

“Muziki siyo mkojo kusema ukijisikia kukojoa ukojoe, bali muziki unahitaji kujipanga sisi wakongwe hatufanyi muziki kama hawa wasanii wa sasa bali sisi wakongwe tunajipanga ili kuachia kazi nzuri kwa mashabiki zetu” alisema Dudubaya

Mbali na hilo Dudubaya alikanusha tetesi za kuwa ubinafsi wake ndiyo ulikuwa chanzo kundi lako la Dar Skendo kufa bali amedai kuwa yeye alihama kutoka Tanzania na kuanza kuishi Uganda hivyo wasanii wenzake aliyowaacha Tanzania ndiyo walishindwa kuliendeleza kundi hilo na kupelekea kufa.

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version