Msanii Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa ametoa sababu ya yeye kupenda kusaidia wasanii ambao wana kiwango cha kati, na kusema anafanya hivyo ili kujitengenezea njia.
Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema anapoamua kufanya ‘collabo’ na wasanii wadogo, hufanya hivyo kwa ajili ya amaisha yake ya kesho kwenye game, ili wakiwa wasanii wakubwa waweze kumshika mkono iawapo ataanguka.
“Mi huwa nashirikisha vijana wakiwa katika kiwango cha kati kabla hawajafika juu kabisa, kama nilivyowashirikisha kina Diamond, kina Mr. Blue walikuwa kiwango cha kati kati kabla hawajafika viwango vyao sasa hivi, nafanya hivyo kwa future yangu, kwa sababu naweza nikawatengeneza wakawa juu kabisa na nikawategemea baadaye wakiwa kama wanamuziki wakubwa wakaniona kaka yao”, alisema DUlly Sykes
DUlly Sykes aliendelea kusema kuwa aliamua kumshirikisha Harmonize kwenye wimbo wake mpya, kwani anaamini Harmonize ni msanii ambaye ana kiwango kizuri kwa sasa, na anaweza kufika mbali kimataifa.
“Harmonize ni mkali kati ya vijana wakali ambao nimewaangalia wanaweza kufika mbali, ndiyo maana nikaamua kumshirikisha”, alisema Dully Sykes.
eatv.tv
Comments
comments