Dully Sykes Afunguka Kumkubali Zaidi Diamond Kuliko Wasanii Wengine
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka sababu ya kumkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko wasanii wengine.
Muimbaji huyo ameiambia Times FM kuwa anamkubali zaidi Diamond kwakuwa amekuwa akimheshimu zaidi.
“Watu wanalalamikaga ‘oooh’ namsifia sana Diamond, nisiongee uongo nakubali wote wananiheshimu lakini Diamond ananiheshimu na kunionesha nidhamu zaidi,” amesema Dully.
Dully ameongeza kuwa kuna kipindi Diamond aliwahi kuinama mbele za watu na kumfunga kamba zake za viatu zilizokuwa zinafunguka.
Bongo5