-->

Duma Afungukia Kufanya Uchafu na Uwoya

MUUZA nyago kwenye muvi za Kibongo, Daud Michael ‘Duma’ juzi kati alipobanwa juu ya kufanya uchafu na muigizaji mwenziye Irene Uwoya kwenye muvi ya Bei Kali kwa kunyonyana ndimi na midomo hadharani alisema kuwa huo si uchafu bali walikuwa kazini na walitakiwa kuonesha uhalisia zaidi.

 

Akipiga stori na gazeti hili, Duma aliendelea kuwa muvi hiyo ni kwa ajili ya watu wazima lakini hata wandani wao, kwa upande wa kila mmoja wao yeye pamoja na Uwoya wanatakiwa kuelewa kwamba pale ni kazini na wawasamehe kwa walichokifanya.

“Kiukweli mimi sioni ubaya wa kilichofanyika pale. Sanaa ni kazi na unapokuwa kwenye scene unatakiwa kuonesha uhalisia zaidi, hicho ndicho kilichotokea na kikubwa muvi ile ni ya watu wazima,” alimaliza Duma.

 

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364