Baada ya kufanya vizuri katika filamu ya mfadhili wangu sasa anakuja kivingine hapa namzungumzia Daudi Michael (Duma) anakuja na filamu yake mpya ambayo imeshutiwa mikoa miwili dar na morogoro, Inaitwa (Mchongo Sio ) ambayo ameshirikiana na mastaa wenzake kibao kama Haji salum (Mboto) Kulwa Kikumba (Dude) Riyama Ally Mzee Kolongo Lukey Lukam…Rucky Baby Mwahija Mvungi na wengineo kibao.
Akiongea na Bongo Movies.com Duma aliwataka mashabiki wa filamu hapa bongo kukaa mkao wa kula kwani anaamini kuwa kazi hii itakonga nyoyo za mashabiki wengi.
Comments
comments