Upande wa Bongo Movie nako kunazidi kuwaka moto ambapo safari hii tena hali inazidi kuwa ya balaa juu ya uwepo wa bifu wa Mwigizaji aliyetamba na tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael “Duma” pamoja na Gabo Zigamba.
Kwa mujibu wa Duma anasema, Katika watu wa kwanza wanaoongoza kuharibu sanaa ya Bongo Movie ni Gabo na sababu anayosema ni kuwa hajitambui.
“Huyu jamaa ni kirusi katika tasnia yetu, angalia kwa mfano amepata tuzo karibia nne,lakini ukiangalia haeleweki mpaka sasa amefanya nini yaani hata ukimuona anapita huwezi kudhani kama ni staa wa filamu sababu hajui kuvaa,” alisema.
“Gabo hana chakuongea, hata watu wanamuogopa kumuita katika sherehe mbalimbali. Mtu gani anaweza kurudia suti zaidi ya mara tatu yani yupo yupo tu anauza sura yaani haeleweki, kifupi kawaangusha Watanzania,” aliongeza zaidi.
Upande wa Gabo akijibu tuhuma hizo anasema kwake hayupo tayari kumuongelea Duma kwa sababu yeye kaamua kumjadili.
“Sinaga urafiki kwanza na mwana taaluma ambaye tunafanana naye, ila upo ujamaa tu lakini kwangu maneno hayana nafasi sana zaidi ya kazi.
“Akili ukiitumia vizuri unaweza kufanya mambo mengi ya maana, hivyo si muda tutaona kipi ni kipi sababu mimi sijali sana maneno anayoongea yeye, mimi nipo kikazi,” alisisitiza.
Comments
comments