Ebitoke Alizwa na Ben Pol (Audio)
Mchekeshaji maarufu bongo Ebitoke alizwa na kitendo cha anayedaiwa kuwa mpenzi wake Ben Pol kutopokea simu wala kujibu meseji zake, na kuomba msaada kwa watu kumuuliza msanii huyo kwa nini anafanya hivyo, licha ya kuwa na mipango mingi ya baadae.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amesema kitendo hicho kinamuweka njia panda, hivyo anashindwa kujua kama anampenda kweli au alikuwa anachezea moyo wake.
Msikilize hapa chini Ebitoke akifunguka zaidi juu ya jambo hilo