Esha Alia Wivu kwa ‘Hausigeli’ Wake
STAA wa filamu za Kibongo, Esha Buheti ‘amelia’ wivu kwa mfanyakazi wake wa ndani (hausigeli) kuwa katika maisha yake ya ndoa hapendi kumwachia ampikie mumewe kwani siyo maadili.
Akizungumza na Showbiz Xtra Esha alisema kuwa, hata mumewe akipikiwa na dada wa kazi huwa anajua kwani akikionja chakula tu lazima aulize mpishi ni nani kutokana kuwa na ladha ya tofauti. “Simwachii dada ampikie mume wangu, chakula chake napika mwenyewe labda niwe naumwa,” alisema Esha.
Chanzo: GPL