Artists News in Tanzania

Faiza Ally Afunguka Kutamani Kuzaa Tena na Sugu

AMEJIZOLEA umaarufu mkubwa kwenye tasnia ya mitindo na filamu hapa nchini, mwingi wa matukio na vituko vyake ambavyo vinashangaza na kuaacha watu wakiwa midomo wazi, huyu ndiyo Faiza Ally, mrembo ambaye itakubidi utenge muda wa ziada ili upate kumuelewa.

faiza7332

Faiza Ally

Huwenda ulikuwa humfahamu lakini habari za kutoka kimapenzi na hatimaye kuzaa mtoto anayeitwa Sasha na mkongwe wa muziki wa  Hiphop nchini, Joseph Mbilinyi Sugu’, zilikufanya uanze kumfuatilia kwa ukaribu ingawa yeye anasema filamu yake itakayotoka hivi karibuni inayoitwa Baby Mama Drama aliyocheza yeye, mtoto wake na Gabo itakufanya shabiki umuelewe vizuri.

Wiki hii Swaggaz, limemuweka kikaangoni, Faiza Ally na atakwenda kutoa majibu ya maswali tata uliyokuwa unajiuliza kuhusu kazi zake, maisha, mapenzi na malezi ya mtoto wake, twenzetu…

SIYO RAHISI KUZAMA PENZINI

Unaweza ukadhani Faiza ni mwanamke anayenasa kirahisi kwenye mitego ya wanaume wanaomtaka kimapenzi. Ipo tofauti sana kwani kabla hajaingia kwenye uhusiano na mtu ni lazima ajiridhishe kama una mambo hayo aliyoeleza hapo chini.

“Kwanza ni lazima anivutie na nijisikie kuwa naye, awe na utu pia sipendi mwanaume ajidhatiti sana kwangu kwa sababu najua muda wowote ninaweza kuachana naye. Kuhusu tabia huwa ninapenda kujiridhisha mwenyewe na siyo kusikia kwa watu,” anasema Faiza.

TETESI ZA KUUZA ‘UNGA’

Juni 3 mwaka huu, Faiza kupitia ukurasa wake wa picha, alitoa malalamiko ya kuvamiwa na askari polisi wapatao saba wakiwa na silaha huku wakimtuhumu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, askari hao walipitisha msako nyumba nzima bila mafanikio, mrembo huyu anafunguka chanzo za kuhisiwa kuwa anauza ‘unga’.

“Nadhani watu tumekuwa tukiishi kwa kukariri, hatupendi kuona maisha ya mtu yamebadilika ndiyo maana wakaenda kutoa taarifa za uongo polisi kuwa nauza dawa za kulevya. Hiyo ilitokana na mimi kusafiri kwenda Kenya na China mara kwa mara kuchukua mzigo kwa ajili ya biashara yangu ya nguo za ndani na ufukweni,” anasema.

 

MUZIKI KIDOGO, KUOGELEA KWA SANA

Idadi ya picha za mrembo huyu kwenye mitandao wa kijamii zimetawaliwa na zile za ufukweni. Huonekana akiwa kwenye fukwe mbalimbali akila bata, hii ina maanisha hapendi muziki na michezo mingine? Kama anapenda muziki basi ni msanii gani ana mkubali ukiacha Diamond Platnumz na Ali Kiba? Anafunguka..

“Muziki naupenda kiasi, huwa nasikiliza nyimbo za TID, sipendi kabisa mpira wa miguu mimi ni mwendo wa kuogelea tu. Kwa upande wa Ali Kiba na Diamond kila mtu anafanya vizuri kwa upande wake, Diamond ana burudisha na Ali Kiba anatoa ujumbe zaidi kwenye nyimbo zake,” anasema Faiza.

KINACHOMPA HUZUNI, FURAHA

“Jambo linalonipa huzuni mara kwa mara ni pale mwanangu Sasha anaponiuliza habari za baba yake, huwa naumia mno. Ila tukio la furaha ambalo siwezi kulisahau ni pale nilipopata uchungu wa dakika kadhaa lakini nilikuja kupata furaha ya maisha yangu yote siku nilipo jifungua, Sasha,” anasema.

SAKATA LAKE NA SUGU

Juni 19 mwaka jana, Faiza alifikishwa kwenye mahakama ya Mwanzo Manzese jijini Dar es salaam na mzazi mwenzie Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, aliyetaka apewe haki ya kumlea mtoto wake Sasha, baada ya kudai kuwa makuzi ya mtoto huyo yanaathiliwa na matendo ya mama yake.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mfawidhi, Patrick Vaginga iliamuru, Sasha akalelewe na baba yake na ikawa hivyo ila haukupita muda mrefu, Sasha alikabidhiwa tena kwa mama yake. Unaweza ukajiuliza kwanini mrembo huyu anaona, Sugu hakustahili kumlea mtoto wao?, mwenyewe anafunguka hapo chini.

“Mimi ninaona hawezi kumlea kama ninavyotaka mimi kwa kuwa ana kosa muda. Maisha ya Sugu muda mwingi hatulii nyumbani kutokana na mambo yake ya siasa, sasa nitamkabidhi vipi mtoto amlee wakati nazijua mishe mishe zake?

Pia alisema mtoto anaweza kwenda kulelewa na Bibi yake huko Mbeya, ninachujua mimi mama yake hawezi kumlea Sasha kwa sababu yeye mwenyewe aliwahi kuniambia kuwa hataki mtoto wake akae kwa bibi yake,” anasema.

CHANZO CHA KUTENGANA

“Mimi na baba Sasha hatukuwahi kugombana niliamua kutengana naye na kuondoka nyumbani kwake, ikawa hivyo tu hatuna ugomvi wowote,” anasema.

PENZI LAKE JIPYA

Baada ya kuachana na Sugu maisha ni lazima yaendelee, Faiza, anasema hivi sasa ametulizwa na penzi la raia wa Marekani huku nguvu zake nyingi akizielekeza kwenye biashara ya nguo za ndani na filamu.

KWANINI ANAPENDA KUZAA TENA SUGU?

Yupo kwenye uhusiano na mtu mwingine ila mipango yake ya kuongeza mtoto imeangukia tena kwa Sugu, japo kuwa hana mapenzi naye. Hapo unaweza ukajiuliza anawezaje kushiriki tendo la ndoa na mtu asiyempenda? Faiza anaelezea..

“Nieleweke kuwa sitamani kuishi naye ila natamani nizae naye mtoto wa pili, unajua leo au kesho mwanangu Sasha atahitaji mdogo wake binafsi napenda  yeye na mdogo wake wawe damu moja.

Siyo hivyo tu, Mungu naye ana mipango yake anaweza akanichukua leo kisha Sasha na mdogo wake wakatengana kutokana na kuzaliwa na baba tofauti, ndiyo maana nasema natamani mtoto wangu wa pili nizae tena na Sugu ili hata nikifa leo najua hawata pata tabu kwa sababu baba yao ni mmoja,” anasema Faiza.

VIPI KUHUSU MAVAZI?

Moja ya vituko ambavyo mrembo huyu amewahi kuvifanya ni kuvaa pampasi siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa pamoja na matukio mengine aliyowahi kuyafanya kwa nyaka tofauti. Kipi kinaKipi kinamsibu avae mavazi hayo?

“Huwa navaa ninavyojisikia, simuigi wala kumsikiliza mtu yoyote, ninachoamua kukivaa navaa, ilmradi nionekane tofauti na nipendeze, mara nyingi huwa navaa vazi lolote linaloniweka komfotabo,” anasema.

Mtanzania

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments

Exit mobile version