Fid Q Amweka Hadharani Mpenzi Wake
RAPA Fareed Kubanda ‘Fid Q’ ameamua kujilipua kwa kumweka hadharani mpenzi wake mapema katikati ya wiki hii kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Katika kile kinachoonekana kufuata nyayo za washkaji zake, FA na AY walioamua kuwaweka hadharani wapenzi wao, Fid Q ameonekana kujiachia na mpenzi wake huyo kwa kupiga selfie kwa kujiachia.
Moja ya picha zilizotikisa mitandao ya kijamii inayomwonyesha Fid Q akiwa na mpenzi wake huyo ambaye ni mgeni machoni pa watu wengi, aliandika, “Blessed beyond measure.”
Mtanzania