-->

Filamu ya Gate Keeper Kuzinduliwa Suncrest Sinema Dar

MTAYARISHAJI na muongozaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Vincent Kigosi kupitia kampuni yake ya R J kwa kushirikiana na Steps Entertainment Ltd itarajia kuzindua filamu kali na ya kusisimua ya Gate Keeper katika ukumbi wa Suncrest Cinema uliopo Mwalim Nyerere.

Sinema hiyo itazinduliwa tarehe 3.3. 2017 huku ikiambatana na matukio makubwa kama vile Red Carpet, watu mashuhuri ambao wapo katika nyanya mbalimbali huku nguli huyo ambaye ndio alama ya filamu akija na big Surprise kubwa kwa wapenzi wa filamu .

Sinema hiyo ambayo imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia kama vile Single Mtambalike , Irene Uwoya, Kajala

Masanja, Haji Adam, Hidaya Njaidi, Richard Masinde, na wasanii wengine wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu kiingilio ni Tshs. 10,000 na show itaanza saa moja usiku.


Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364