Filamu ya Gharika Baada ya Miaka 3 Sasa Kuingia Sokoni
FILAMU ya Gharika ni filamu ambayo imetumia muda mwingi katika kuhakikisha inatoka katika ubora wa hali ya juu kwani ni hadithi iliyogusa maisha ya watu walikufa maji huko Zanzibar jambo ambalo lilizidisha uhalisia kwa sinema hiyo iliyotengenezwa na Mohamed Mwikongi.
Ni kazi iliyochukua nafasi kubwa ya muda wangu kwani awali ilikuwa ni imeitwa Spice island lakini nikashauri nibadili jina kwani kuna matukio ya ukweli yanayosisimua na kufundisha hiyo ndio filamu ya Gharika,”anasema Frank
Filamu ya Gharika imekamilika na ipo tayari na inaingia sokoni kesho siku ya Ijumaa na kusambazwa nchi nzima katika maduka ya filamu za Kibongo na inasambazwa na Steps Entertainment.
Katika filamu ya Gharika kuna wasanii wakali wa sinema Swahilihood ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu wakiongozwa na Frank, Ben Blanco na wasanii wanaofanya vizuri katika game.
FC